PIGA KURA

PIGA KURA

Wednesday, July 20, 2016

MEYA JACOB AMKARIBISHA DC POLEPOLE


Amwambia anasubiri busara imwongoze kama aende Ubungo ama abaki Kinondoni na akienda ni kwa ajili yake. 




MSTAHIKI MEYA wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob leo katika kikao cha baraza la madiwani, amemkaribisha Mkuu wa Wilaya mpya ya Ubungo Humphrey Polepole kuwasalimia madiwani hao kabla ya mgawanyo huo.

Awali kabla ya Polepole kuingia ukumbini, Meya Jacob alisema kwamba taratibu za serikali  kugawanya manispaa ya kinondoni kuwa na ya Ubungo zinakamilika na wakati wowote, Wilaya hiyo inaweza kuanza kazi.



"Kama ambavyo tume ya uchaguzi ilianza michakato yake ya kugawa majimbo na hatimaye jimbo la ubungo likagawanywa na kupata kana jimbo la kibamba kulingana na wingi wa watu wake...
Ndiyo serikali kuu (Tamisemi)ili tangazo kuwa Wilaya ya ubungo na michakato ya kugawa Mali, mapato na  watumishi yaliendelea na sasa tayari sehemu kubwa yamekamilika hata jengo la manispaa, muda wowote watumishi na madiwani watatakiwa kwenda huko" alisema Meya Jacob

Hata hivyo akimkaribisha DC Polepole alisema " karibu sana Wilaya ya Ubungo

...mimi bado sijasema niende au nibaki wapi, nasubiri busara iniongoze hivyo tuko pamoja maana wote ni wamoja ila nikija huko ni kwa ajili yako jiandae"



NAYE DC Polepole akiwasalimia madiwani wa manispaa ya Kinondoni alisema kuwa angetamani Wilaya ya Ubungo iwe ya tofauti katika uongozi wake endapo kila kiongozi na mtumishi atafaa kazi kwa maendeleo ya nchi.

"Mh rais amenichagua nije katika wilaya mpya ya ubungo na nitoke msoma vijijini kwa malengo na kazi ile ile ya wakuu wote wa wilaya ya ulinzi na usalama wa wilaya husika lakini pia kwa ajili ya dhamana ya kusimamia sera na ustawi wa maendeleo hivyo tufanye shughuli zetu kwa amani"

" Kwa wanaonifahamu vizuri mie ni mwanaccm kweli kweli na siyo wa bahati mbaya, lakini naheshimu demokrasia ya ustawi wa vyama vingi na kufanya kazi na watu wengi kwani si mara ya kwanza kufanya kazi na viongozi wa upinzani ....nimefanyanao bila kuvunjiana heshima"  alisema Polepole

DC Pole pole alisema kwamba anategemea siasa ya maendeleo katika wilaya hiyo na siyo siasa ya madaraka kwa kuwa msingi mkubwa wa kuwapo  viongozi na watumishi ni maendeleo kwa eneo husika.
MBUNGE wa Kinondoni Maulid Mtulia (CUF)alimshukuru DC Polepole kwa elimu hiyo na kumuahidi kwamba kama ataweka mbele maslahi nchi basi watashirikiana  naye bila migongano yoyote baina yao na yeye, watumishi na serikali kuu

"Nafikiri tuendelee na  kazi ya kutafanya siasa ya maendeleo ili baadae tupate siasa ya madaraka ... ili mkiwa mnaitengeneza Ubungo ya tofauti, siye kinondoni tubaki na kinondoni ya pekee"


Mapema akijibu hoja za madiwani kuhusu shughuli za maendeleo za manispaa hiyo alisema watatumia wataalamu kufanya utafiti na kushauri ili kuhakikisha wanaondoa changamoto za kujenga barabara Chini ya kiwango.
"Suala la barabara ni la kitaalamu hivyo linapaswa kuangaliwa kwa makini na sio kulaumu watu waliopita tunaanza upya na kuendelea mbele...kwa sasa tutakuwa tukipima kwanza ili kuondoa matatizo yaliyokuwapo awali" alisema Meya Jacob

Aidha alisema barabara za akachube, mabatini, Mikocheni na zingine ziliharibika haraka kutokana na kutumia lami nyepesi na maeneo hayo kuwa na chemchem ya Maji.

"Tusiwalaumu wakandarasi kwani wanajenga barabara kulingana na kiwango cha fedha walichopewa ambapo katika manispaa hii tunatoa milioni 400 kwa kilomita moja wakati hao hao wanajenga za wakala wa barabara nchini Tanroads na haziharibiki kwa kuwa wanapewa fedha za kutosha" alisema.

MEYA WA KINONDONI APOKEA MSAADA WA MADAWATI 100

* Awataka wahisani wengine kujitokeza kusaidia.

Mstahiki Meya wa Halimashauri ya Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob Leo amepokea msaada wa madawati 100 toka Shirika la Social Action Trust Fund (SATF)lenye makazi yake Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Meneja Program wa SATF Rogasian Massue

Akizungumza katika hafla hiyo fupi Meya Jacob alisema kwamba mpango ulipo kwa Manispaa hiyo nikuhakikisha hadi mwezi Agosti mwaka huu, hakuna mwanafunzi atakayekaa chini kutokana na kuwa na uwezo wa kuwatosheleza.


"Nawashukuru sana nyie Shirika la SATF kwa msaada wenu huu kwetu Manispaa... tunawaalika wadau wengine wa elimu kutuletea msaada mwingine wa madawati ili yajae na mengine tuweke stoo akiba ili watoto watakapovunja wapewe mengine maana ni watundu sana" alisema
Pamoja na hilo Meya Jacob   aliwataka wadau wengine wa elimu kujitokeza kutoa msaada wa madawati kwa kuwa uhitaji wake bado upo.

Hata hivyo alisema kuwa mpaka sasa wazabuni waliopewa kazi ya kutengeneza madawati zaidi ya 16000 wanaendelea ili yaanze kugawiwa kwa shule za Manispaa hiyo haraka. 

Mapema Meneja Program wa SATF Rogasian Massue alisema kuwa watoa madawati yao 100 kama mpango wao wa kusaidia wilaya mbalimbali ili vijana waweze kupata elimu na kuwa wataalam mbalimbali.

Massue alisema katika program ya kutoa msaada wa madawati 150 katika  Halmashauri ya Chato mkoani Geita, wakafuatilia Kinondoni jijini Dar es Salaam madawati 100. 


Meneja program huyo alisema sasa wanajiandaa kupeleka msaada Manispaa za Temeke na Ilala za hapa jijini, wilaya ya Kankonko mkoani Kigoma na  Kaliua  mkoani Tabora.  


Imeandaliwa na Janet Josiah.

Tuesday, July 5, 2016

MSTAHIKI AFUTURISHA KINONDONI

Mstahiki Meya Boniface Jacob afuturisha Kinondoni.
Aendeleza utamaduni ulioachwa na Londa, Mwenda.


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob jana Julai Mosi amefutulisha,wananchi wa manispaa hiyo wakiwamo wadau na wanasiasa wa vyama vyote,hafla iliyofanyika katika viwanja hivyo. 
Akizungumza katika shughuli hiyo,  Mstahiki Meya alisema Manispaa yake ipo  imara kuliko inavyotarajiwa pamoja na kuwepo vikwazo vya   hapa na pale.
Akifafanua kauli yake,alisema pamoja na serikali kuu kuchukua tozo yote ya majengo ambayo ni zaidi ya sh bilioni 10 ambayo itakusanywa na TRA,tayari manispaa hiyo imeshajipanga kukusanya kiasi hicho kwa njia nyingine.
"Kama miezi sita  sasa tumeweza kufanya vizuri kuliko manispaa zote...hivyo hatutashindwa kukusanya mapato na kuleta maendeleo.
"Sitaki kuwa mnafiki mwezi  huu mtulya wa Ramadhan,  kuna vikwazo vingi Kama mnavyosikia na kujionea ila tutavishinda kwa uwezo wake Mungu.
Pamoja na hayo Mstahiki Meya  alitoa zawadi ya viwanja vitano vilivyopo Mabwepande kama sadaka kwa makundi yenye mahitaji maalum (walemavu,yatima,mashirika ya dini,watoto wanaolelewa katika Ngo's) kama sadaka toka manispaa hiyo vitakavyotolewa kwa utaratibu kuandika barua ya maombi kwa mkurugenzi .
Hata hivyo aliwashukuru wote walifika kushiriki futari na kueleza kwamba ataendelea kula nao katika kipindi cha miaka mitano kama walivyokuwa wakifanya mameya waliopita Londa na Mwenda.

CUF - Mwakalishi wake katika shida alisema kuwa hata kama serikali imezuia kufanyika mikutano, huo ni  uoga wao, wao kama ukawa watafanya.

 CCM Mwakalishi alimshukuru  mstahiki Meya kwa mwaliko wa masheikh bila ubaguzi.

CHADEMA Mwakilishi alisema hali ya maisha ime badilika sana hata kufanya waislam wafuturu kwa shida na Chadema itaendelea kupiga kelele.

MBUNGE Mwakalishi wa Kinondoni Mtulia alisema wabunge wa manispaa ya kinondoni wote wanne (ubungo,kawe,kibamba na kinondoni) wanamasikitiko  makubwa sana kwa kuwa wametolewa matumaini ya kuwapa maendeleo wananchi waliyoahidi baada
ya serikali kuchukua tozo ya majengo ambayo ndiyo chanzo kikubwa.
Sheikh Katimba alisema hii  nchi yetu sote ambayo inaendeshwa na demokrasia lakini hawaelewi kwanini kuna ubakwaji wa demokrasia.

"Tunawaomba wakubwa waache wabunge wafanye kazi yao..."alisema

Aliongeza kwamba bajeti ya sasa ime kuwa  ngumu na hapo hapo serikali kuzuia mitumba kuingia nchini hali inayosababisha ugumu wa maisha hata wananchi kushindwa kununua nguo za sikukuu kama walivyoshindwa kununua sukari kipindi hiki cha ramadhan.
Sheihk Katimba aliitaka serikali iache kukurupuka katika uamuzi wake na kufuatilia jambo mpaka mwisho.

Alitoa mfano wa kweli ambao alisema unawaumiza waislam wengi na kwa dini yao kupinga wa wenzao kuitwa magaidi hata kuwekwa gerezani bila ya uchunguzi kukamilika na kuwakamata wanaofatilia,.

"Tunaiomba serikali  irekebishe hali hii ya sasa kwani wimbo wa amani aukamiliki bila haki...Innah..."

Mwisho. Imeandikwa na Janet Josiah.

MEYA BONIFACE JACOB AKABIDHI TIMU KWA WANANCHI

Mstahiki Meya Boniface Jacob akabidhi timu kwa wananchi.
Afanya mazungumzo na wadau wa soka Kinondoni. 


HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imekabidhi timu ya soka ya manispaa hiyo KMC FC kwa wananchi kwa ajili kuisaidia ishiriki michuano ya Ligi Kuu Tanzania bara.



 Hatua hiyo inatokana na timu hiyo inayoshiriki Ligi daraja la kwanza kutofanya vizuri kwa miaka mitatu mfululizo tangu inunuliwe.

 Akizungumza jijini Dar es Salaam leo na wadau wa soka wa manispaa hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob alisema mwenendo mbaya wa timu hiyo imesababisha ishindwe kufika mbali. 

Alisema kutokana na mwenendo huo, manispaa hiyo imeamua kuwakutanisha wadau wa soka ili kuwakabidhi timu.

 "Awali tulikuwa hatujafanya hivyo ila tumeonelea tuirudishe kwa wananchi ili wapate fursa ya kutoa mchango wao, licha ya kuwa usimamizi wa masuala ya bajeti utakuwa chini ya halmashauri," alisema. Meya Jacob  ambaye pia ni alike wa  Mwenyekiti wa kikao.hicho, alibainisha kuwa licha ya timu hiyo kugharamiwa kwa kila kitu lakini bado imekuwa haifanyi vizuri. "Tumekosa fursa mbalimbali ikiwemo ya timu yetu kwenda jijini Humburg Ujeruman, endapo tungefanya vizuri ama kupanda daraja kushiriki Ligi Kuu," alisema. Katika mkutano huo ulioudhuliwa na wadau mbalimbali, walieleza kuwa kushuka kwa timu hiyo kunatokana na kutoshirikishwa kwa wananchi muds.mrefu. Mdau wa soka, Ramadhan Kampira alisema kuwa lazima iundwe kamati ya wataalam ili kuisimamia timu hiyo ndani na nje ya uwanja. "Haya yote.yanafanyika lakini tutambue tumechelewa sana, ilatakiwa mipango ianze muda mrefu hatuwezi kufanya usajili ndani ya wiki tatu kisha tuamini tutafika Ligi Kuu," alisema. Mdau mwingine, Idd Mbonde alisema kuwa timu hiyo ilikosa utawala bora wa kuisimamia ndio maana imekuwa ikifanya vibaya. "Kinachotakiwa kufanyika sasa hii timu wakabidhiwe wananchi angalau kwa miaka miwili ili tuhakikishe inafanya vizuri," alisema



Hata hivyo Meya Jacob alimaliza kikao hicho kwa kuunda kamati ya uongozi ya watu 12 wataohakikisha wanasimamia usajili wa wachezaji,katiba na uchaguzi wa  uongozi wa kudumu. Imeandikwa na Janet Josiah