PIGA KURA

PIGA KURA

Wednesday, July 20, 2016

MEYA JACOB AMKARIBISHA DC POLEPOLE


Amwambia anasubiri busara imwongoze kama aende Ubungo ama abaki Kinondoni na akienda ni kwa ajili yake. 




MSTAHIKI MEYA wa Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob leo katika kikao cha baraza la madiwani, amemkaribisha Mkuu wa Wilaya mpya ya Ubungo Humphrey Polepole kuwasalimia madiwani hao kabla ya mgawanyo huo.

Awali kabla ya Polepole kuingia ukumbini, Meya Jacob alisema kwamba taratibu za serikali  kugawanya manispaa ya kinondoni kuwa na ya Ubungo zinakamilika na wakati wowote, Wilaya hiyo inaweza kuanza kazi.



"Kama ambavyo tume ya uchaguzi ilianza michakato yake ya kugawa majimbo na hatimaye jimbo la ubungo likagawanywa na kupata kana jimbo la kibamba kulingana na wingi wa watu wake...
Ndiyo serikali kuu (Tamisemi)ili tangazo kuwa Wilaya ya ubungo na michakato ya kugawa Mali, mapato na  watumishi yaliendelea na sasa tayari sehemu kubwa yamekamilika hata jengo la manispaa, muda wowote watumishi na madiwani watatakiwa kwenda huko" alisema Meya Jacob

Hata hivyo akimkaribisha DC Polepole alisema " karibu sana Wilaya ya Ubungo

...mimi bado sijasema niende au nibaki wapi, nasubiri busara iniongoze hivyo tuko pamoja maana wote ni wamoja ila nikija huko ni kwa ajili yako jiandae"



NAYE DC Polepole akiwasalimia madiwani wa manispaa ya Kinondoni alisema kuwa angetamani Wilaya ya Ubungo iwe ya tofauti katika uongozi wake endapo kila kiongozi na mtumishi atafaa kazi kwa maendeleo ya nchi.

"Mh rais amenichagua nije katika wilaya mpya ya ubungo na nitoke msoma vijijini kwa malengo na kazi ile ile ya wakuu wote wa wilaya ya ulinzi na usalama wa wilaya husika lakini pia kwa ajili ya dhamana ya kusimamia sera na ustawi wa maendeleo hivyo tufanye shughuli zetu kwa amani"

" Kwa wanaonifahamu vizuri mie ni mwanaccm kweli kweli na siyo wa bahati mbaya, lakini naheshimu demokrasia ya ustawi wa vyama vingi na kufanya kazi na watu wengi kwani si mara ya kwanza kufanya kazi na viongozi wa upinzani ....nimefanyanao bila kuvunjiana heshima"  alisema Polepole

DC Pole pole alisema kwamba anategemea siasa ya maendeleo katika wilaya hiyo na siyo siasa ya madaraka kwa kuwa msingi mkubwa wa kuwapo  viongozi na watumishi ni maendeleo kwa eneo husika.
MBUNGE wa Kinondoni Maulid Mtulia (CUF)alimshukuru DC Polepole kwa elimu hiyo na kumuahidi kwamba kama ataweka mbele maslahi nchi basi watashirikiana  naye bila migongano yoyote baina yao na yeye, watumishi na serikali kuu

"Nafikiri tuendelee na  kazi ya kutafanya siasa ya maendeleo ili baadae tupate siasa ya madaraka ... ili mkiwa mnaitengeneza Ubungo ya tofauti, siye kinondoni tubaki na kinondoni ya pekee"


Mapema akijibu hoja za madiwani kuhusu shughuli za maendeleo za manispaa hiyo alisema watatumia wataalamu kufanya utafiti na kushauri ili kuhakikisha wanaondoa changamoto za kujenga barabara Chini ya kiwango.
"Suala la barabara ni la kitaalamu hivyo linapaswa kuangaliwa kwa makini na sio kulaumu watu waliopita tunaanza upya na kuendelea mbele...kwa sasa tutakuwa tukipima kwanza ili kuondoa matatizo yaliyokuwapo awali" alisema Meya Jacob

Aidha alisema barabara za akachube, mabatini, Mikocheni na zingine ziliharibika haraka kutokana na kutumia lami nyepesi na maeneo hayo kuwa na chemchem ya Maji.

"Tusiwalaumu wakandarasi kwani wanajenga barabara kulingana na kiwango cha fedha walichopewa ambapo katika manispaa hii tunatoa milioni 400 kwa kilomita moja wakati hao hao wanajenga za wakala wa barabara nchini Tanroads na haziharibiki kwa kuwa wanapewa fedha za kutosha" alisema.

No comments:

Post a Comment