* Awataka wahisani wengine kujitokeza kusaidia.
Mstahiki Meya wa Halimashauri ya Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob Leo amepokea msaada wa madawati 100 toka Shirika la Social Action Trust Fund (SATF)lenye makazi yake Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Meneja Program wa SATF Rogasian Massue
Akizungumza katika hafla hiyo fupi Meya Jacob alisema kwamba mpango ulipo kwa Manispaa hiyo nikuhakikisha hadi mwezi Agosti mwaka huu, hakuna mwanafunzi atakayekaa chini kutokana na kuwa na uwezo wa kuwatosheleza.
"Nawashukuru sana nyie Shirika la SATF kwa msaada wenu huu kwetu Manispaa... tunawaalika wadau wengine wa elimu kutuletea msaada mwingine wa madawati ili yajae na mengine tuweke stoo akiba ili watoto watakapovunja wapewe mengine maana ni watundu sana" alisema
Pamoja na hilo Meya Jacob aliwataka wadau wengine wa elimu kujitokeza kutoa msaada wa madawati kwa kuwa uhitaji wake bado upo.
Hata hivyo alisema kuwa mpaka sasa wazabuni waliopewa kazi ya kutengeneza madawati zaidi ya 16000 wanaendelea ili yaanze kugawiwa kwa shule za Manispaa hiyo haraka.
Mapema Meneja Program wa SATF Rogasian Massue alisema kuwa watoa madawati yao 100 kama mpango wao wa kusaidia wilaya mbalimbali ili vijana waweze kupata elimu na kuwa wataalam mbalimbali.
Massue alisema katika program ya kutoa msaada wa madawati 150 katika Halmashauri ya Chato mkoani Geita, wakafuatilia Kinondoni jijini Dar es Salaam madawati 100.
Meneja program huyo alisema sasa wanajiandaa kupeleka msaada Manispaa za Temeke na Ilala za hapa jijini, wilaya ya Kankonko mkoani Kigoma na Kaliua mkoani Tabora.
Imeandaliwa na Janet Josiah.
No comments:
Post a Comment