KMC -FC yainyuka SIMBA FC 1-0
Bao la dakika ya 11 liliwekwa wavuni na Rashid Roshwa wa timu ya Manispaa ya Kinondoni leo lilitosha kuizamisha Simba katika mchezo wa kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Highland uliopo Chuo cha Bibilia Mkoani Morogoro.
Simba ikiwa na kikosi kamili ilishindwa kusawazisha bao hilo licha ya jitihada za washambulizi wake wakiongozwa na ibrahim Ajibu na Danny Lyanga.
KMC - FC walionekana kuikamia mechi hiyo tangu mwanzo wa mchezo wakifanya mashambulizi ya kushtukiza na kufanikiwa kulilinda bao hilo hadi mwisho wa mchezo.
KMC - FC wanaendelea na mazoezi kesho katika viwanja vya Bora- Kijitonyama kujiandaa na mechi nyingine ya kirafiki Ijumaa JKT Ruvu viwanja vya Mbweni.
Pongezi nyingi zimuendee Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob kwa kujitoa kwa hali na mali ili kurudisha nguvu na heshima ya michezo kwenye Manispaa ya Kinondoni hususani kwenye kuiendeleza timu ya mpira wa miguu ya KMC - FC.
Imeandikwa na Janet Josiah
No comments:
Post a Comment