PIGA KURA

PIGA KURA

Saturday, August 6, 2016

Meya Boniface Jacob atoa vyeti kwa wasaidizi wa ustawi wa jamii Kinondoni.



MSTAHIKI wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Boniface Jacob jana 28/7/2016 alifunga mafunzo ya wasaidizi ustawi wa jamii 237 na kutoa vyeti kwa  washiriki hao.

Washiriki hao 237 walipatiwa mafunzo ya siku 10 jijini Dar es Salaam ili kukabiliana na janga la Ukimwi na hasa kwa kutazama makundi maalum ambayo kwa namna  moja ama nyingine,   hayakupewa kipaombele (watoto walio katika mazingira hatarishi).

Akizungumza katika hafla hiyo, Meya Jacob alisema kuwa Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na madiwani wake, imejipanga kulipa kulipa msukumo mkubwa kwa kuwa athari zake kwa jamii ni kubwa.

Meya Jacob aliwataka wasaidizi hao wa ustawi wa jamii kuhudumia kwa moyo na bila ubaguzi kwa kuwa kazi ya kuhudumia jamii haichagui Dini, ukabila wala itikadi za kisiasa.

"Nawaombeni sana mlio patiwa mafunzo haya,   wakiwemo maafisa ustawi wa jamii na wengine wa ngazi ya Kata  na nyie mliojitolea kwamba jambo hili ni letu hivyo ni lazima tulisimamie kwa nguvu zetu zote ili tufikie kiwango kizuri cha udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa kuwashawishi upimaji wa VVU" alisema

Meya Jacob aliwashukuru waandaaji wa mafunzo hayo John Snow Inc (JSI) chini ya mradi wa uimarishaji mifumo ya afya na ustawi  wa jamii ambao unafadhiliwa na watu wa  marekani, shirika la FHI360 kwa kushikiana na shirika la WAWATA.

Naye Mkurugenzi wa mafunzo ya ustawi wa jamii  kutoka Chuo Cha Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam Leah Omary alisema kuwa Chuo hicho kinajivunia kutoa mafunzo hayo ambayo ufanikiwa katika jamii iliyotuzunguka.

Akitoa shukrani kwa mafunzo hayo, Mmoja wa washiriki hao, Ally Firina,  alisema kwa kuwa viongozi wa mitaa yao waliwaamini na kuwapa nafasi ya kujifunza namna ya kutoa huduma kwa jamii kama wasaidizi wa ustawi wa jamii, wananchi watoe ushirikiano ili kuweza kuleta mabadiliko ya haraka na chanya.

Imeandikwa na Janet Josiah.

No comments:

Post a Comment